Propellerads

Baada ya kuzinguana na Guardiola, Yaya Toure afunguka ukweli wake kwa mara ya kwanza



Mchezaji bora Afrika mara nne, Yaya Toure amevunja ukimya wake
tangu atolewe katika kikosi cha UEFA klabuni Manchester City na kocha Pep Gaurdiola.

Kapteni huyo mstaafu wa Ivory Coast bado anafanya mazoezi na kikosi cha kwanza Man City japokua Guardiola alitoa kauli kwamba hatompanga tena mpaka wakala wake atakapoomba radhi kwa maoni yake kwenye vyombo vya habari.

Baada ya kipindi cha mazoezi jana Jumanne, Toure alifunguka kupitia mtandao wa Twitter kwamba ni ngumu kwake.

"Kipindi kizuri cha mazoezi asubuhi hii. Vigumu kutocheza klabu bingwa. Lakini nadhani wenzangu wapo vizuri kwa kesho (leo)." ali tweet.


Kwa mujibu wa ESPN, nyota huyo alikua na furaha kipindi cha mazoezi ambapo vyombo vya habari vilipewa nafasi kwa dakika 15 za mwanzo pekee.





Baada ya kuzinguana na Guardiola, Yaya Toure afunguka ukweli wake kwa mara ya kwanza Baada ya kuzinguana na Guardiola, Yaya Toure afunguka ukweli wake kwa mara ya kwanza Reviewed by Steve on Wednesday, September 28, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.