Kuhusu Zlatan kuanza leo, Mourinho amesema hivi
Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kwamba
Zlatan Ibrahimovic ataanza mchezo wa leo wa Europa katika kundi A dhidi ya Zorya Luhansk.
Mapema wiki hii ilidaiwa kwamba nyota huyo alipewa ruhusa ya kutocheza mechi hiyo kuelekea mchezo wa wikiendi dhidi ya Stoke City.
Hata hivyo Mourinho amefunguka katika mkutano wa kabla ya mechi akisema Zlatan ataanza baada ya kuulizwa endapo Mswedeni huyo ataanza mechi ya leo.
Luke Shaw hatakuwemo kwenye mchezo wa leo kutokana na majeraha, lakini Mourinho amethibitisha Anthony Martial amepona majeraha yake ambayo yalisababisha kukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Leicester.
Kuhusu Zlatan kuanza leo, Mourinho amesema hivi
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 29, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment