Barcelona na Neymar kuchunguzwa tena
Uhalali wa mchezaji huyo kuhama mwaka 2013 kuja Barca akitokea Santos ya Brazil umekua katika utata mwingi tangu awasili.
Inaaminika ada ya uhamisho iliyotangazwa haikua sahihi na sasa La Liga wamethibitisha kwamba watafanya uchunguzi wao huku kesi ya kwanza ikiwa imeshasikilizwa ambapo klabu hiyo ya Catalunya ikikiri makosa.
"Kufuatia kuenea habari mbali mbali, La Liga imethibitisha kua uchunguzi utafanyika kwa Barcelona kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kati ya ofisi ya mwendesha mashitaka na bodi ya klabu kuhusu kesi ya Neymar" tangazo rasmi lililotolewa na La Liga.
Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu mapema mwaka huu alikubali kulipa faini ambayo ilionesha klabu hiyo kukiri makosa, lakini ni bado kidogo kesi hiyo kumalizika kabisa.
Barcelona na Neymar kuchunguzwa tena
Reviewed by Steve
on
Friday, September 16, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment