Propellerads

Antonio Conte afichua kwanini hampangi Fabregas kikosi cha kwanza



Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amefichua kwanini mchezaji wa zamani
wa FC Barcelona, Cesc Fabregas hampangi katika kikosi chake cha kwanza.

Kiungo huyo mhispania amecheza dakika 26 pekee katika Premier League chini ya kocha mpya Chelsea akiwa nyuma ya Nemanja Matic, Oscar na N'Golo Kante nafasi ya kiungo wa kati Chelsea.

Sasa kocha Antonio Conte amefafanua kwanini hampi nafasi katika kikosi cha kwanza huku akisisitiza kwamba mchezaji huyo bado klabu ina mipango nae.

"Cesc yupo katika mipango yangu na mipango ya Chelsea," alisema Conte kama alivyonukuliwa na Daily Star.

"Kwa mtazamo wangu, anaendelea kua bora kwenye mambo mengi.

"Kama akiendelea hivi, itakua ngumu kwangu kuchagua kiungo. Lakini nataka hivi kutoka kwa mchezaji, kunipa wakati mgumu katika kuchagua.

"Niko wazi katika wachezaji wangu, kama mchezaji anastahili kucheza ninamweka kwenye timu."


Antonio Conte afichua kwanini hampangi Fabregas kikosi cha kwanza Antonio Conte afichua kwanini hampangi Fabregas kikosi cha kwanza Reviewed by Steve on Friday, September 16, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.