Kikosi kinampa Mayanja kiburi, hebu ona anachotaka sasa kutoka kwa TFF!!
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amedai kuwa wao Simba wapo tayari
kupewa ruhusa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba kikosi hicho kichezeshwe michezo miwili kwenye ratiba yao kutokana na upana wa wachezaji walionao katika msimu huu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayanja alisema wanaomba hivyo kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji wanaokaa benchi na jukwaani nao kuonyesha sehemu ya uwezo wao.
“Kama inawezekana sisi tuchezeshwe mechi mbili yaani moja hapa Dar na nyingine mkoani kwa ajili ya kuwapa nafasi wale wasiocheza na wanaokaa benchi nao kuonyesha viwango vyao.
“Wakikubali sisi wala hatuna hofu kwa sababu tuna kikosi kikubwa ambacho kinaweza kutimiza jambo hilo na bila kupata tatizo kwenye timu yoyote ile,” alisema Mayanja.
Kikosi kinampa Mayanja kiburi, hebu ona anachotaka sasa kutoka kwa TFF!!
Reviewed by Steve
on
Friday, September 16, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment