Antonio Conte atoa sababu iliyowagharimu Chelsea mbele ya Liverpool
Bosi wa Chelsea, Antonio Conte amedai kwamba
kukosa umakini ndio kumeigharimu timu yake kupoteza mbele ya Liverpool kwa 2-1 jana Ijumaa usiku.
The Blues walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao mawili kabla ya mapumziko pamoja na Diego Costa kufunga bao kipindi cha pili lakini bado hawakuweza kuambulia pointi yoyote kwenye mchezo huo.
"Kutafuta sababu muda mwingine ni rahisi na muda mwingine ni vigumu. Magoli yalikua ya kushtukiza. Tunatakiwa tuhisi hatari lakini leo hatujafanya hivyo.
"Tunatakiwa kujifunza zaidi kutoka kwenye huu mchezo ili kuelewa hali endapo hatutaki kurudia msimu mbaya kama uliopita.
"Kipindi cha pili pressure ilikua nzuri. tulijitahidi na kucheza vizuri lakini unatakiwa kua makini kama unafikiria kuhusu timu nzuri."
Antonio Conte atoa sababu iliyowagharimu Chelsea mbele ya Liverpool
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 17, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment