Kompany: Man City sio klabu kubwa

Vincent Kompany amedai kua Manchester City hawawezi kujiita
'klabu kubwa' mpaka wakishinda Champions League.
Klabu hiyo imejitahidi kuchukua karibia kila mataji ya nyumbani tangu 2011-yakiwemo mawili ya Premier League, lakini wameonekana kutofanya vizuri kwenye mpira wa Ulaya.
City walitolewa katika michuano ya mikubwa Ulaya na Barca ndani ya miaka miwili iliyopita ambapo Kompany anasema ubingwa Ulaya ni muhimu kwa kupata jina kubwa.
"Ni kitu cha mwisho tunachotakiwa kukipata ili kuthibitisha kua tumekua klabu kubwa," alisema Mbelgiji huyo kama alivyonukuliwa na The Mirror.
Endapo wakiwafunga Sevilla Jumanne ijayo, City watafuzu hatua ya pili ya michuano.
Kompany: Man City sio klabu kubwa
Reviewed by Steve
on
Monday, November 02, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment