Matokeo yote VPL michezo ya jana
Ligi kuu tanzania bara imeendelea jana kwa michezo
mitano kupigwa kwenye viwanja vitano tofauti, ukiachana na mchezo kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-1 kwenye uwanja wa Taifa matokeo mengine yalikuwa kama ifuatavyo.
Azam FC imeendeleza ushindi na kuendelea kukimbizana na Simba na Yanga baada ya leo kuifunga timu ya Mwadui FC kwa goli 1-0 mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’. Agrey Morris alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mwadui kuzawadiwa penati lakini mshambuliaji wa Mwadui Rashid Mandawa alishindwa kukwamisha wavuni mkwaju huo wa penati.
Kwenye uwanja wa Manungu mjini Morogoro Mtibwa walikuwa wenyeji wa Ndanda FC na Mtibwa imefanikiwa kushinda kwa goli 2-1 dhidi ya Ndanda FC.
Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Salim Mbonde dakika ya kipindi cha kwanza na Said Bahanuzi akafunga goli la pili kwa upande wa Mtibwa Sugar huku goli pekee la Ndanda likifungwa na Kigi Makasi.
Mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Toto Africans umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kutofungana kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Matokeo yote VPL michezo ya jana
Reviewed by Steve
on
Monday, September 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 21, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment