Propellerads

Hii hapa sababu kwanini Van Gaal alimtoa Matteo Darmian dhidi ya Southampton



Louis Van Gaal ameelezea kwanini alichukua maamuzi ya kumtoa beki
wake Matteo Darmian dhidi ya Southampton ambapo walishinda 3-2.

Wikiendi hii haya ndio matokeo ligi kubwa za Ulaya

Beki huyo wa kulia kutoka Italia, alijiunga na United majira ya joto kwa thamani ya pauni mil 12.7 akitokea Torino alitolewa katika half time na nafasi yake akaingia Antonio Valencia.

Lakini Van Gaal anadai hakumtoa sababu ya majeraha na anasisitiza ilikua ni kimbinu zaidi.

Kama alivyonukuliwa na Express alisema "Yalikua ni mabadiliko ya kimbinu kwa sababu Tadic alikua na nafasi sana na ilikua ni hatari kwetu. Nilitaka kuondoa hilo kwa kumtumia Valencia na alifanya vizuri nadhani"

Bosi huyo wa Red Devils ameonekana kumkubali sana Matteo Darmian ambapo amekua akianza karibia kila mechi tangu awasili Old Trafford.

Hii hapa sababu kwanini Van Gaal alimtoa Matteo Darmian dhidi ya Southampton Hii hapa sababu kwanini Van Gaal alimtoa Matteo Darmian dhidi ya Southampton Reviewed by Steve on Monday, September 21, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.