Kumbe Wenger aliamua 'kuichinjia' dili ya Cavani!!
Imedaiwa kua Arsenal waliamua kuachana na dili la
mshambuliaji wa PSG, Edinson Cavani katika dakika za mwisho.
Kwa mujibu wa The Mirror, kocha wa Gunners Arsene Wenger aliamua kuachana na dili hilo baada ya kile kilichodaiwa Cavani hajaendana na thamani ya bei aliyokua amewekewa.
Kuelekea kufungwa kwa usajili jana, Arsenal waliripotiwa kua na matumaini ya kuwapata Edinson Cavani au Karim Benzema ili kuongeza nguvu ya ushambuliaji, lakini mambo yameenda ndivyo sivyo.
Kwa hali hiyo Petr Cech ndio mchezaji pekee aliyesajiliwa na Gunners msimu huu pamoja na kwa kwamba wamedaiwa kua na pesa za kutosha kwa sasa.
Kumbe Wenger aliamua 'kuichinjia' dili ya Cavani!!
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 02, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 02, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment