Dili za usajili Ulaya zilizofanyika jana siku ya mwisho
Galatasaray wammesainisha Kevin Grosskreutz kutoka
Borussia Dortmund kwa ada ya £1.5m.
Norwich City wamemsainisha winga, Matt Jarvis, kwa mkopo wa muda mrefu kutoka West Ham United.
Liverpool wamemtoa kwa mkopo beki wao, Tiago Illori, kwenda Aston Villa kwa msimu wa 2015/2016..
Everton wametangaza kumsaini winga, Aaron Lennon, kwa dili la miaka mitatu akitokea Tottenham Hotspur.
Leicester City wameongeza nguvu ya ushambuliaji kwa kumsaini Nathan Dyer kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Swansea City.
AFC Bournemouth wamethibitisha kumsaini beki Joe Bennett kwa mkopo mpaka January.
Napoli wamemsaini kiungo wa England, Nathaniel Chalobah, kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Chelsea.
FC Porto wamethibitisha kumsaini kiungo Mmexico, Miguel Layún, kutoka Watford.
Chelsea wamemtoa kwa mkopo, Islam Feruz, kwa klabu ya uskochi, Hibs, mkopo wa muda mrefu.
Watford wametangaza kumsainisha mchezaji wa kimataifa wa Algeria, Adlène Guedioura,kutoka Crystal Palace kwa dili la miaka mitatu..
Watford wamemsainisha mkolombia Victor Ibarbo, kwa mkopo wa muda mrefu kutoka AS Roma.
Manchester United wamethibitisha kumnasa Anthony Martial kutoka AS Monaco kwa dau la £36m.
Sunderland wamekamilisha usdajili wa DeAndre Yedlin kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Tottenham Hotspur.
West Ham United wamethibitisha kumsajili Michail Antonio akitokea Nottingham Forest kwa mkataba wa miaka minne.
Aston Villa wamemsaini aliyekua beki wa Manchester City Joleon Lescott kwa mkataba wa miaka miwili.
Chelsea wametangaza kumsajili beki Msenegal Papy Djilobodji kutokea Nantes kwa mkataba wa miaka minne.
Aston Villa wamethibitisha kumsajili kipa wa Anderlecht Matija Sarkic katika dili la miaka mitatu.
Southampton wamemsajili beki mdachi, Virgil van Dijk kwa ada ya £11.5 million mkataba wa miaka 5 akitokea Celtic.
Bournemouth wamemsajili mshambuliaji Glenn Murray katika dili la miaka mitatu.
West Ham nao walithibitisha kumsaini Nikica Jelavic kwa miaka miwili akitokea Hull City.
West Ham wao wamemnasa Victor Moses kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Chelsea.
Deportivo La Coruna wamemsaini Jonas Gutierrez kutoka Newcastle kwa uhamisho huru.
Everton wamekamilisha dili la beki Ramiro Funes Mori kwa ada ya£9.5m kutoka River Plate kwa mkataba wa miaka 5.
West Ham United kupitia mmiliki mwenza David Gold wamethibitisha kumpata Alex Song kwa mkopo.
Dili za usajili Ulaya zilizofanyika jana siku ya mwisho
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 02, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 02, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment