Propellerads

Wenger atoa sababu kwanini Giroud alikua benchi kwenye mechi ya Newcastle



Olivier Giroud wa Arsenal alikua benchi kwenye mechi dhidi ya
Newcastle kwenye uwanja wa St James Park .

Badala yake nafasi yake ilichezwa na Theo Walcott ambapo kocha Arsene Wenger amedai kua lilikua ni swala la mbinu ili kuendana na mchezo wa Newcastle.



"Ndio bila shaka, wao (Giroud na Walcott) wana ubora tofauti na ndio maana muda mwingine kwenye michezo bmingine ninamweka Giroud na mingine Walcott. Ni washambuliaji wakubwa kwa hiyo tutumaini kwamba nimefanya maamuzi sahihi."

Mesut Ozil pia hakuwemo kwenye kikosi kutokana na majeraha kidogo kwenye goti, hata hivyo hajawahi kucheza Newcastle tangu awasili Arsenal mwaka 2013.

Mlinzi wa Arsenal  Laurent Koscielny, jana alirejea kikosini baada ya kupona majeraha lakini Mertesacker hakuemo kutokana na kuumwa.

Wenger alifanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi cha jana ukilinganisha na kile cha mechi ya Liverpool ambapo  Koscielny, Alex Oxlade-Chamberlain na Walcott walianza badala ya Calum Chambers, Ozil na Olivier Giroud.

Kwenye mechi hiyo ya Premier league jana Arsenal walishinda 1-0, bao la kujifunga la  Fabricio Coloccini dakika ya 52.

Wenger atoa sababu kwanini Giroud alikua benchi kwenye mechi ya Newcastle Wenger atoa sababu kwanini Giroud alikua benchi kwenye mechi ya Newcastle Reviewed by Steve on Sunday, August 30, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.