Propellerads

Maneno ya Mourinho baada ya kipigo cha Crystal Palace leo



Jose Mourinho amesema timu yake ilistahili ushindi kwenye
mechi ya leo dhidi ya Crystal Palace ambayo wameshindwa kwa 2-1 wakiwa nyumbani Stamford Bridge.



Bao la Joel Ward  katika dakika ya 81 ndio liliizamisha Chelsea ambayo mudakidogo kabla ilikua imesawazisha bao la kwanza kupitia Radamel Falcao.

Kwenye mechi hii, Chelsea wamepata mashuti 26 huku tisa pekee ndio yakilenga golini ambapo Mourinho anasema sare ndiyo ilikua wanaistahili kwa mchezo wa leo.



"Hongera kwao Palace. Ni matokeo mazuri kwao na perfomance nzuri" aliiambia BBC SPORT.

"Hatukustahili kupoteza. Lakini Palace wametupa mchezo mgumu. Matokea yalitakiwa iwe sare ,ambayo isingekua mbaya kwetu. Tumepambana vya kutosha."




Baada ya kupoteza mechi ya leo, sasa Chelsea wako nyuma ya point nane kwa Man City ambao wameendelea kujihakikishia ushindi wao kwa asilimia 100 baada ya kuwapiga Watford 2-0.

Maneno ya Mourinho baada ya kipigo cha Crystal Palace leo Maneno ya Mourinho baada ya kipigo cha Crystal Palace leo Reviewed by Steve on Saturday, August 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.