Thomas Muller asema hajafanya mawasiliano yoyote na Van Gaal
Nyota wa Bayern Munich, Thomas Muller amekanusha
kua hajafanya mawasiliano yoyote na kocha Louis van Gaal kufuatia uvumi wa kwamba anataka kujiunga na Manchester United.
Tetesi zilizopo kwa sasa ni kua Man United wamemtengea Muller dau la pauni mil 71 mshambuliaji huyo ambaye ameripotiwa pia kuvutiwa na uhamisho huo.
Huko Ujerumani iliripotiwa kua Van Gaal ambaye amepata kumfundisha Muller Bayern Munich, amefanya mawasiliano nae jambo ambalo amelikanusha.
"Louis van Gaal hajanipigia, kwa hiyo sijui kuhusu uhamisho wowote " aliwaambia waandishi wa Ujerumani baada ya kufunga magoli mawili jana kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Bayern Leverkusen.
Muller ana mkataba Allianz Arena mpaka mwaka 2019.
Thomas Muller asema hajafanya mawasiliano yoyote na Van Gaal
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 30, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment