Propellerads

Wenger aongea kuhusu majeraha ya Wilshere, hawezi kumbadilisha




Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka kua hawezi kubadilisha aina
ya uchezaji ili kupunguza kiasi cha majeraha ambayo humtesa nyota huyo.

Wilshere mwenye miaka 23, anaweza kukosa wiki nane za mwanzo kwa timu yake msimu huu kutokana na kuandamwa na majeraha miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo, Wenger anaamini Wilshere ambaye amepata kuanza michezo chini ya 50 tu ya EPL tangu 2011 hawezi kubadilisha aina yake ya mchezo ambayo imeonekana ndio chanzo kikubwa cha yeye kuumia.

"Huwezi kucheza mpira bila kujiachia" Wenger alifunguka kama alivyonukuliwa na SKY Sport News

"Mchezo wa Jack ni wa kuweka mpira mguuni na kupenya,. Kama ukizuia hiyo, unambadilisha mchezaji na unakua umemtolea moja ya vitu vinavyompa uwezo sana uwanjani"

The Gunners wataanza mbio za EPL kwa kuwakaribisha West Ham kesho jioni.

Wenger aongea kuhusu majeraha ya Wilshere, hawezi kumbadilisha Wenger aongea kuhusu majeraha ya Wilshere, hawezi kumbadilisha Reviewed by Steve on Saturday, August 08, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.