Mourinho afafanua kuhusu hofu juu ya usajili na kutetea taji
Jose Mourinho amekubali kua kukosekana kwa usajili wa maana na wa
kutosha Chelsea inaweza kua hatari kwa klabu kutetea taji lake la EPL.
Wenger afunguka kuhusu majeraha ya Wilshere
Kocha huyo mreno amedai kua wachezaji wake wanatakiwa kua makini zaidi msimu huu baada ya wao kushindwa kuwanasa wachezaji iliokua wamewakusudia kabla ya kuanza kwa Premier League.
Walikua na ofa mbili kwa ajiliu ya John Stones ambazo zote zilikataliwa, hawajapata beki wa kushoto lakini tayari wamewaingiza Asmir Begovic na Radamel Falcao tkuziba nafasi za Petr Cech na Didier Drogba walioondoka msimu huu.
Yote hayo yanatokea, wapinzani wakubwa wa Chelsea, kama vile Arsenal na Man United tayari wamefanya usajili muhimu,
"Ni hatari, nadhani kama unavyosema ni sawa" Mourinho aliiambia Telegraph
"Lakini hata hawa waliopo wanaweza kusonga. Hauhitaji kununua wachezaji 10 ili uwe na kikosi kizuri. Timu inaweza kua bora na wachezaji wapya wawili au watatu na hata ambao tayari wapo"
Mourinho afafanua kuhusu hofu juu ya usajili na kutetea taji
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 08, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment