Van Gaal amfagilia kipa wake Romero
Louis van Gaal amesema mashabiki watarajie mambo makubwa
kutoka kwa kipa wao Sergio Romero ambaye ameanza vizuri msimu huu.
Kufuatia minong'ono iliyotawala juu ya Davi De Gea ambaye inasemekana yuko mbioni kutua Real Madrid kabla ya kufungwa dirisha la usajili, ilimlazimu kocha mholanzi kumleta Romero Old Traford kwa uhamisho huru.
Romero ameonesha makali yake kwa kuokoa hatari nne katika michezo mitano na sasa kocha anaamini kipa huyo atakua mkali zaidi akifanya majaribio kila siku.
"Nadhani ameokoa maeneo muhimulakini mpaka sasa ile hatari dhidi ya Brugge iliikua muhimu zaidi, pia alisaidia sana kwenye mechi na Tottenham" van Gaal aliwaambia waandsishi.
"Kwa hiyo hawezi kujionesha kwa kile anachokifanya, lakini ni jukumu lake kwa timu. Tusingemnunua kama hatumwamini"
United wataumana na Swansea ugenini Jumapili hii.
Van Gaal amfagilia kipa wake Romero
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment