Pamoja na yote, Mourinho ana imani kubwa na kikosi chake
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kua ana
imani kubwa tu na kikosi chake pamoja na kuwepo taarifa za kutaka kuwasajili Pogba na John Stones.
Ripoti zinadai kua The Blues inaweza kuwasajili wachezaji hao wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Everton, usiku uliopita walitangaza kukataa ofa ya Chelsea huku tayari kulikua na nyingine tatu zilizokataliwa pia kwa ajili ya John Stones.
Pamoja na kuonekana kua na udhaifu kwenye safu yake ya ulinzi, Mourinho amewaambia waandishi " Kama nikipata mchezaji mwingine mwishoni mwa usajili vizuri, kama nikikosa kikosi nilichonacho ni kizuri"
Chelsea leo wanawakaribisha Crystal Palace nyumbani Stamford Bridge.
Pamoja na yote, Mourinho ana imani kubwa na kikosi chake
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment