Tetesi: Man United kumtengea ofa ya £73m Arjen Robben??!!
Manchester United wanatarajia kuweka ofa ya
pauni mil 73 kwa ajili ya winga wa Bayern Munich, Arjen Robben hii ni kwa mujibu wa ripoti.
Uvumi huu unakuja baada ya Red Devils kumkosa Pedro ambaye alijiunga na Chelsea siku kadhaa zilizopita.
Gazeti la Daily Express limeripoti kua kocha Louis van Gaal anataka kusajili mshambuliaji kabla ya kufungwa dirisha la usajili jumanne ambapo anafikiria kumpata Robben ambaye amepata kumfundisha katika kipindi akiwa kama kocha wa Uholanzi.
Majira haya ya joto mpaka sasa Man United wamefanikiwa kusajili wachezaji watano, ambao ni Morgan Schneiderlin, Memphis Depay, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger ana Sergio Romero.
Tetesi: Man United kumtengea ofa ya £73m Arjen Robben??!!
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 29, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment