Propellerads

Real madrid sasa kumsainisha De Gea kwa kiasi hiki



Real Madrid wameripotiwa kukaribia kumsainisha
David de Gea kwa kiasi cha pauni mil 29.

Raia huyo wa hispania mwenye miaka 24 amekua akihusishwa na Real Madrid karibu kipindi chote hichi cha usajili, na yuko tayari kuondoka Man United msimu huu.

The Independent limeripoti kua tayari Real Madrid wametuma maofisa wake kwenda Manchester kukamilisha dili hilo huku makubaliano binafsi na mchezaji yakiwa yameshakamilika.

Pia gazeti hilo limezidi kuripoti kua Los Blancos hawana mpango wa kumjumuisha nyota wake Gareth Bale kama sehemu ya dili.

De Gea amecheza michezo 131 akiwa na Man United huku akichukua taji la ligi chini ya Sir Alex Ferguson msimu wa 2012/13.
Real madrid sasa kumsainisha De Gea kwa kiasi hiki Real madrid sasa kumsainisha De Gea kwa kiasi hiki Reviewed by Steve on Sunday, August 30, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.