Neymar ataja nyota watatu ambao angependa kucheza nao kikosi kimoja
Nyota wa FC Barcelona, Neymar ametaja nyota watatu ambao angependa kucheza
nao kikosi kimoja, huku miongoni mwao wakiwemo wakongwe wawili wa Real Madrid.
Nyota huyo aliwataja wachezaji hao baada ya kuulizwa wakati akifanya mahojiano na FIFA TV
"Mimi ni mshabiki mkubwa wa Romario, ni mchezaji ambaye napenda ningeweza kucheza nae" alisema Neymar
"Pia Zidane. Ronaldo nilicheza nae katika mechi yake ya mwisho na Brazili, lakini napenda ningeweza kucheza nae zaidi.
"Hao ndio wachezaji ambao ningependa kucheza nao kikosi kimoja" alimaliza.
Neymar ataja nyota watatu ambao angependa kucheza nao kikosi kimoja
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 16, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 16, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment