Propellerads

Maamuzi ya Mavugo baada ya kutemwa na Simba



Mshambuliaji wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo, sasa amethibitisha
kwa 100% kufa kwa dili lake na Simba baada ya kurejesha fedha za awali alizopewa na Wekundu hao.

Mavugo ambaye awali alionyesha kutoafiki suala la kurejesha fedha hizo akiamini lolote linaweza kutokea, amebadili mawazo na kurudisha ‘advance’ ya dola 10,000 (Sh milioni 20) aliyotanguliziwa na Simba kwa makubaliano ya kumaliziwa dola 10,000 nyingine baada ya kusaini.

Dili la Mavugo na Simba lilikufa baada ya Vital’O kuongeza dau la usajili la mchezaji huyo kutoka Sh milioni 120 mpaka 200 baada ya kuelezwa kuwa timu kibao zinamtolea udenda, hiyo ikaifanya Simba kukaa kando na kuangalia mipango mingine.

Mtu wa ndani wa Simba amelivujishia Championi Ijumaa ishu hiyo na jinsi walivyoahidiana na Mavugo kama itatokea wakati mwingine wakihitaji huduma yake.

“Ameturejeshea ile pesa tuliyompa bila ya tatizo na tumemalizana naye, tumeelewana kuwa kama baadaye tunaweza kuhitaji huduma yake basi tutakamilisha hilo kwa wepesi zaidi maana hata hatukuelewa kilichotokea kwa Vital’O kwenye dakika za mwisho,” alisema bosi huyo.

Maamuzi ya Mavugo baada ya kutemwa na Simba Maamuzi ya Mavugo baada ya kutemwa na Simba Reviewed by Steve on Friday, August 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.