Propellerads

Louis van Gaal amesema hawata 'panic' kununua wachezaji.



Kocha wa Man United amesema kupoteza mechi yake ya
jana dhidi ya Swansea kwa 2-1 hakuwezi kumfanya ku panic na kuanza kunbunua katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya kufungwa dirisha la usajili.

Magoli mawili ndani ya muda mfupi kutoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi Gomis yalibadilisha kabisa hali ya mchezo na kuifanya Swansea kuongoza  kwani Man United kabla walikua mbele kwa bao moja lililofungwa na Juan Mata dakika ya 48.

Baada ya kuwakosa Pedro na Nicolas Otamendi wiki iliyopita, Red Devils wanaweza kuchangamka kabla ya kufungwa dirisha la usajili jumanne, lakini van Gaal amesisitiza kipigo cha Swansea sio sababu ya kumfanya aongeze wachezaji.

"Hapana, haina madhara yoyote" aliiambia Sky Sports.

"Kununua mchezaji au kutonunua sio sababu kua tume panic mchezo uliopita"

"Kama uliangalia mchezo, nadhani tuliutawala lakini tulitakiwa kufunga zaidi"

Mpaka sasa Man United wamewasajili  Memphis Depay, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin na Sergio Romero
Louis van Gaal amesema hawata 'panic' kununua wachezaji. Louis van Gaal amesema hawata 'panic' kununua wachezaji. Reviewed by Steve on Monday, August 31, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.