Juan Mata afunguka baada ya kipigo cha Man United jana
Kiungo wa Man United, Juan Mata amesema kua makosa ndani ya
dakika tano yaliigharimu timu yake kwa kupoteza kwa 2-1 mbele ya Swansea jana.
Mata aliifungia Man United goli la kuongoza dakika ya 48 kabla ya Andre Ayew na Bafetimbi Gomis kuipatia ushindi Swansea.
Mhispania huyo anaamini kua walishindwa kuendana na mchezo baada ya kusawazishiwa na kuongezwa hali iliyowafanya kupoteza mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza.
"Ni dissapoitment sana" aliiambia Sky Sports "Tulifanya kitu kigumu, ambacho ni kufunga kwanza tukaongoza lakini ndani ya dakika tano tukapoteza mchezo .
"Walibadilika na tulishindwa kuendana nao. Wali react vizuri wakatufunga magoli mawili haraka haraka"
United sasa wako nafasi ya tisa katika msimamo wa Premier League baada ya michezo minne.
Juan Mata afunguka baada ya kipigo cha Man United jana
Reviewed by Steve
on
Monday, August 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 31, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment