Propellerads

Baada ya ofa nyingine tena kukataliwa, Chelsea wajipanga kupata mbadala wa John Stones



Everton wametolea nje tena ofa nyingine ya Chelsea ya
pauni mil 37 kwa beki wake John Stones.

Kwa sasa Chelsea wameamua kuachana na swala la mchezaji huyo baada ya ofa hii ya nne sasa kukataliwa ambayo ilikua inavunja rekodi ya uhamisho kwa mabeki.

Tayari Everton walishachomoa ofa zingine za  £20m, £25m na £30m kutoka kwa Mourinho.

The Blues walipeleka ofa yao ya mwisho jumanne hii ambayo pia ni siku hiyo hiyo Stones naye alituma ombi la kuondoka klabuni hapo ambapo  pia klabu ilikataa.

The Express wanadai kua kwa sasa Chelsea wameamua kuelekeza nguvu kwa wakali wengine kama vile Raphael Varane wa Real Madrid, Muarjentina Ezequiel Garay wa St Petersburg ambao wanaweza kua mbadala wa Stones.

Stones alisajiliwa Everton mwaka 2013 kwa pauni mil 3 akitokea Oakwell.
Baada ya ofa nyingine tena kukataliwa, Chelsea wajipanga kupata mbadala wa John Stones Baada ya ofa nyingine tena kukataliwa, Chelsea wajipanga kupata mbadala wa John Stones Reviewed by Steve on Friday, August 28, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.