Baada ya kutemana na Msenegal, Simba waleta mwingine kutoka Mali
Simba imeendelea na mchakato wake wa kusaka mshambuliaji ‘muuaji’ baada ya
kumshusha nchini Makan Dembele raia wa Mali.
Dembele tayari amepelekwa Zanzibar kuungana na wachezaji wengine wa Simba walio huko ili apate nafasi ya kumuonyesha Kocha Dylan Kerr kwamba yeye ni nani na ana uwezo upi.
Tayari mshambuliaji Pape Abdoulaye N’daw raia wa Senegal naye yuko Zanzibar kufanya majaribio na Kerr ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuweka tiki.
Dembele ,29, aliwahi pia kukipiga katika klabu kongwe ya Algeria ya JS Kabylie.
Simba imeachana na mshambuliaji Papa Niang raia wa Senegal pia baada ya kumpa siku mbili za mazoezi pamoja na dakika 45 katika mechi ya kirafiki.
Imekuwa ikihaha kusaka mshambuliaji mara tu baada ya kuachana na Amissi Tambwe ambaye ametua Yanga na kuendelea kutesa.
Baada ya kutemana na Msenegal, Simba waleta mwingine kutoka Mali
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 27, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment