Usajili wa kujutia uliowahi kufanywa na Man United katika historia.
Manchester United wamepata kufanya usajili wa nguvu katika baadhi ya vipindi, mfano wa usajili huo ni kama
vile Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo, lakini kuna usajili ambao ulifanywa ukitegemewa kua wa nguvu lakini mambo yakawa ndivyo sivyo,
Owen Hargreaves
Mchezaji huyu wa zamani wa timu ya taifa ya England alisaini Red Devils May 2007 kwa dau la pauni mil. 17 ambapo alipata kucheza mara 39 pekee katika misimu minne iliyokua ya majeraha kwake klabuni hapo.
Eric Djemba-Djemba
Sir Alex Ferguson alikua na matumaini makubwa wakati akimsajili nyota huyu mwaka 2003, mpaka ilifikia hatua mkameruni huyo akabatizwa Roy Keane mpya, hata hivyo alishindwa kuonesha makali yake. Baada ya miaka miwili aliuzwa.
Radamel Falcao
Ingawa alijiunga Man United kwa mkopo, lakini uhamisho huo haukua na mafanikio sana kwa pande zote. Falcao amefunga magoli manne pekee katika michezo 26 ya Premier League, kocha Van Gaal amechagua kutompa mkataba wa kudumu.
Anderson
Mbrazil huyu alisajiliwa kutoka Porto mwaka 2007, na alikua anaandaliwa kua nyota mkali ndani ya EPL. Hata hivyo Anderson alishindwa kuthamanisha dau lake la pauni mil. 26 ambapo aliondoka kama mchezaji huru baada ya msimu wake wa mwisho.
Juan Sebastian Veron
Akisajiliwa kwa dau la pauni mil 28.1 kutokea Lazio mwaka 2001, Veron alishindwa kabisa kuhimili mikiki mikiki ya Premier League. Alifanikiwa kucheza 82 kwa Man United na alikuja kuuzwa Chelsea kwa kiasi ambacho ilikua kama nusu ya ada aliyonunuliwa.
Usajili wa kujutia uliowahi kufanywa na Man United katika historia.
Reviewed by Steve
on
Friday, July 03, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 03, 2015
Rating:



