Umeisikia hii....Balotelli amehusishwa na kutua TP Mazembe
Liverpool sasa wamefulia, kwani tarifa za sasa ambazo sio rasmi zinadai kua
nyota Mario Balotelli huenda akajiunga na wakali TP Mazembe.
Muitaliano huyo msimu uliopita alikua katika wakati mgumu kurejea katika kiwango chake chini ya kocha Brendan Rodgers na chapisho moja la Ufaransa liitwalo Football France limedai huenda mkali huyo akaingia Afrika.
Balotelli amekua akihusishwa na kutaka kurejea Serie A na mipango mingine mingi tu ya mkopo, lakini sasa imeripotiwa anaweza aka experience maisha ya Congo kwa msimu mmoja.
Kulingana na ripoti, Balotelli alizungumza na meneja wa wakali hao wa Congo, Patrice Cartelon juu ya kufanyika kwa swala la mkopo.
"Nilishangaa siku moja asubuhi kukuta meseji kutoka namba ya Uingereza" Cartelon alisema, kama alivyonukuliwa na Football France
"Mwanzoni nilidhani ni kama utani, kulikua na kasoro katika uandishi, kwani ulikua ni mchanganyiko wa english na kitaliano. Lakini nilipopiga nikagundua ni Balotelli.
"Aliniambia neno kwa neno kua anataka kutua kwa mabingwa wa Afrika, nilicheka lakini nikasema 'ndio'
"Nilimpigia Brendan Rodgers , ambaye nae hakusita kunitumia Mario jioni"
TP Mazembe wanadaiwa kutaka kumtumia Balotelli ili kutete ubingwa wa ligi ya nyumbani baada ya kuupoteza kwa AS Vita msimu uliopita, vile vile kushinda michuano ya CAF.
Balotelli nae amekua akihangaika kuyazoea maisha ya Liverpool, kwani alifunga magoli manne pekee katika michuano mbali mbali msimu uliopita, alipewa ruhusa ya kwenda kwao baada ya kupata msiba, na kwa sasa anafanya mazoezi peke yake klabuni baada ya kikosi kingine kwenda katika ziara ya kabla ya msimu.
Umeisikia hii....Balotelli amehusishwa na kutua TP Mazembe
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 22, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment