Ripoti: Di Maria kuondoka Man United
Aliyekua nyota wa klabu ya Real Madrid, Angel Di Maria ameripotiwa kua
amewaambia Manchester United kua anataka kuondoka klabuni hapo.
Nyota huyu amekua akihusishwa sana kutaka kujiunga na miamba ya Ufaransa, PSG, na sasa anadaiwa kuiomba klabu kama anaweza kuondoka majira haya ya kiangazi.
Di Maria, ambaye alijiunga na mashetani wekundu mwanzoni mwa msimu uliopita amekua akipambana na kukosolewa sana kutokana na kucheza chini ya kiwango japo wengine wanadai kua anahitaji muda zaidi kuzoea mikiki mikiki ya England.
Kuanzia wiki kadhaa zilizopita mkali huyo amekua akihusishwa kwa kiasi kikubwa na PSG, na Starsport wanaamini kua huenda Di Maria akaelekea Paris.
Inaaminika kua wakali wa Ufaransa wako tayari kutenga dau la pauni mil 40 kwa Di Maria, lakini hata hivyo inadaiwa pia Man united nao wanahitaji kiasi karibu na kile walichotumia kumnunua.
Ripoti: Di Maria kuondoka Man United
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 22, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment