Propellerads

Cheki Yanga walivyoua mtu leo na baadhi ya matukio katika picha



Yanga imerejea katika michuano ya Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibout katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.



Katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo, Yanga ilianza kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia huku mshambuliaji wake Donald Ngoma akilambwa kadi ya nyekundu.



Malimi Busungu ndiye shujaa baada ya kufunga mabao mawili huku Geofrey Mwashuya, dogo kabisa akifunga bao la tatu.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa na bao moja lililofungwa na Busungu.



Hata hivyo, Yanga ilikosa mikwaju miwili ya penalti, akianza Amissi Tambwe ambaye mpira aliopiga ulitoka nje, kabla ya Simon Msuva naye kupoteza penalti ya pili.



Yanga sasa itashuka tena dimbani Ijumaa kuivaa KMKM kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.






Katika mechi nyingine KMKM wameanguka mbele ya klabu ya Khartoum ya Sudan kwa mabao 2-0
Cheki Yanga walivyoua mtu leo na baadhi ya matukio katika picha Cheki Yanga walivyoua mtu leo na baadhi ya matukio katika picha Reviewed by Steve on Wednesday, July 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.