Msuva alivyowaambia kina Twite
Kiungo kiraka mpya wa Yanga, Joseph Zuttah kweli noma, kwani anamudu kucheza kwa ufasaha nafasi zaidi ya tatu na kuzua hofu kwa baadhi ya nyota wa timu hiyo.
Zuttah raia wa Ghana ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo, anamudu kucheza vizuri beki na winga ya kulia, kiungo mkabaji na mshambuliaji namba kumi.
Katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, Zuttah ameonekana kumudu kucheza vizuri nafasi hizo ambazo zinachezwa na wachezaji nyota wa timu hiyo.
Juma Abdul anacheza beki ya kulia, Simon Msuva (winga ya kulia) na Mbuyu Twite na Salum Telela, sasa wote kwa pamoja mmoja wao anaweza kupoteza nafasi kumpisha Zuttah acheze.
Akimzungumzia Zuttah, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambaye ndiye aliyeunganisha dili la kuja kwake nchini, alisema: “Zuttah ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi nne ndani ya uwanja na ndiyo maana kila nafasi ninayompanga anacheza vizuri.
“Nilishawahi kusema kuwa Zuttah ana uwezo wa kucheza namba mbili, sita, saba na kumi, sasa hapa Yanga nitampanga popote kutegemea na aina ya mechi tutakayokutana nayo.”
Msuva alivyowaambia kina Twite
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 04, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 04, 2015
Rating:



