Headlines za usajili magazeti ya ulaya leo.
Pogba kuelekea Barcelona.
Paul Pogba amekaribia kuamua kua ni wapi ataelekea baada ya
Juventus, lakini wengine wanadai yuko tayari kukaa Juventus kwa msimu mmoja zaidi kabla hajaelekea Camp Nou baada ya Euro 2016. (L'Equipe)
Sterling kusaini Man City
Manchester City wanatarajiwa kumsainisha nyota wa Liverpool, Raheem Sterling kwa dau la pauni mil 45. Pia wakali wengine kama Paul Pogba, Kevin De Bruyne, na Fabian Delph pia wako katika orodha. (Star Sunday)
Arsenal wako tayari kumtolea pauni mil. 18 Karim Benzema
Real Madrid wako tayari kumuuza Karim Benzema na Arsenal wako tayari kutoa kiasi cha Euro mil 25 (pauni mil 17.5) (Metro)
Man Utd kuingilia dili la Begovic
Chelsea wanahofia Man United wataingilia dili lao la kumnasa Asmir Begovic. The Blues wako katika mazungumzo na Stoke City juu ya bei ya kipa huyo m-boznia, huku van Gaal nae akimuwinda ili kuziba nafasi ya De Gea.(Daily Mail)
Schneiderlin anataka Arsenal
Man United wamekua wakipigana kumnasa nyota wa Southampton, Morgan Shneiderlin, lakini mfaransa huyo yeye mwenyewe ametamka kua angependa zaidi kucheza Arsenal (The Sunday Times)
Man Utd kumuwinda Kane
Man U wamekua na mazungumzo ya moja kwa moja na Tottenham kwa ajili ya kumnasa Harry Kane kwa dau la pauni mil 40. (The Sun)
Austin anasubiri ofa ya Chelsea
Charlie Austine anasubiri ofa kutoka Chelsea kabla hajaamua hatma yake, Mshambuliaji huyo wa QPR amevutiwa na ofa na pesa kutoka Chelsea na hayuko tayari kwenda Leicester City. (The People)
Manchester City wako tayari kutoa pauni mil 50 kwa De Bruyne
Man City wako tayari kutoa dau la pauni mil 50 kwa ajili ya nyota wa Wolfsburg, Kelvin De Bruyne.
(The Sunday Telegraph)
Headlines za usajili magazeti ya ulaya leo.
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 05, 2015
Rating:



