Propellerads

Tetesi: Van Persie na Di maria nje, Bale ndani

Manchester United wanadaiwa kutaka kumsajili nyota kutoka Real Madrid Gareth Bale mwishoni mwa msimu huu na kuwaacha Robin Van Persie na
Angel Di Maria.

Kama klabu itawauza Di Maria na Van Persie, The Mirror limeripoti kua klabu itaokoa kiasi cha pauni 500 000 kwa wiki ambazo ni gharama za mshahara wa Di Maria na Van Persie, hivyo itawawezesha kumfukuzia Bale.


                                       
Van Persie na Di Maria


Ikiwa Di maria hajaonesha mafanikio makubwa ukilinganisha na pesa iliyotumika kumnunua- pauni mil 59.7 na Varn Persie ambaye msimu huu amekaa benchi muda mrefu, klabu inapanga kuwauza ambapo mishahara yao wote ni jumla ya pauni 500 000 kwa wiki.

Kwa upande wa Bale yeye hakua katika kiwango chake msimu huu hali iliyopelekea mashabiki  mara kwa mara kuonesha kukosa imani nae pale Madrid.


                                                                 
Bale


Van Persie amecheza michezo 30 msimu huu ambapo ametoa mchango katika magoli 12, huku Di Maria amecheza michezo 32, amefunga mabao manne na kutoa usaidizi mara 12.

Bale yeye amecheza michezo 47 ,akifunga magoli 17 na kutoa usaidizi mara 12.
Tetesi: Van Persie na Di maria nje, Bale ndani Tetesi: Van Persie na Di maria nje, Bale ndani Reviewed by Steve on Sunday, May 17, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.