Propellerads

Taifa Stars kukipiga na Swaziland:COCAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi Swaziland katika michuano ya
COSAFA.

                                        
Taifa Stars


Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili.
kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika mazingira mazuri.
Akiongelea mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri, mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo anawaandaa vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
Kikosi cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu.
Taifa Stars kukipiga na Swaziland:COCAFA Taifa Stars kukipiga na Swaziland:COCAFA Reviewed by Steve on Saturday, May 16, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.