Simba yamsainisha Ndemla kwa miaka miwili.
Kiungo mahiri wa klabu hiyo, Said Ndemla ameikata maini Yanga iliyokuwa inamnyatia kwa kumwaga wino mkataba wa miaka miwili
Taarifa za ndani za Simba zinasema kuwa, Ndemla amesaini mkataba huo jana mchana na kulipwa kiasi cha Sh 40 Milioni pamoja na gari ili kumtuliza mzuka baada ya kuenea kwa habari kwamba Yanga walikuwa tayari kumalizana na mchezaji huyo chipukizi.
Inaelezwa kuwa Kamati ya Usajili ya Simba ililazimika kumaliza mambo mapema kwa kuhofia kuzidiwa ujanja na Yanga ambayo imekuwa ikimmezea mate kiungo huyo, ambaye tangu apatishwe katika kikosi cha wakubwa toka timu ya vijana amekuwa gumzo kwa soka lake.
Simba yamsainisha Ndemla kwa miaka miwili.
Reviewed by Steve
on
Friday, May 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 15, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment