Barca haoo pamoja na kufungwa jana
WAZEE wa soka la burudani, FC Barcelona wametinga fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-3 dhidi ya FC Bayern Munich ya Pep Guardiola.Mechi ya kwanza Camp Nou, Barcelona walishinda 3-0 na jana usiku wakali hayo wa ‘Katalunya’ wamekufa 3-2 dimba la Allianz Arena mjini Munich
Magoli ya Bayern yalifungwa na Mehdi Benatia dakika ya 7′, Roberto Lewandowski 59′ na Thomas Muller dakika ya 74, wakati nyota wa Brazil, Neymar Jr alifunga magoli yote mawili ya Barcelona dakika za 15′ na 29′ akipokea pazi zote kutoka kwa Luis Suarez.
Ukiachana na matokeo, soka lilikuwa zuri, Bayern walijitahidi kupambana na kumiliki mpira kwa asilimia 54 dhidi ya 46, lakini Barcelona si timu ya kuisogelea kirahisi.
Bayern walifika langoni kwa Barca na kupiga mashuti 8 yaliyolenga lango wakati wageni wao walipiga matano (5) tu.
Kitu cha kushangaza, Barca hawakupiga shuti lolote ambalo halikulenga lango, lakini Bayern waliokuwa na papara walipiga mashuti 10 yasiyolenga lango.
Leo usiku majira ya saa 3:45 Real Madrid wanaikaribisha Juventus ‘Vibibi vya Turin’ katika mechi ya marudiano ya nusu fainali inayopigwa uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mechi ya kwanza uwanja wa Juventus mjini Turini, Real walikufa 2-1 na leo wanahitaja ushindi wa goli 1-0 ili kutinga fainali kwa faida ya goli la ugenini.
Mechi ya kwanza uwanja wa Juventus mjini Turini, Real walikufa 2-1 na leo wanahitaja ushindi wa goli 1-0 ili kutinga fainali kwa faida ya goli la ugenini.
Barca haoo pamoja na kufungwa jana
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 13, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 13, 2015
Rating:





No comments:
Post a Comment