Propellerads

Hatma ya mikataba ya Sanchez na Ozil klabuni Arsenal



Arsenal wana imani kubwa kuendelea kuwa na nyota wawili
Mesut Ozil na Alexis Sanchez katika mikataba ya muda mrefu hivyo kuzima tetesi zote kuhusu hatma yao.

Wawili hao kila mmoja amebakiza miaka miwili katika mkataba wa sasa, lakini kwa mujibu wa The Mirror, watendaji klabuni Arsenal wana mpango wa kuwashawishi nyota hao kusaini tena, huku kwa upande wa Ozil ikionekana kuwasili kwa Shkodran Mustafi ambaye ni swahiba yake ni sababu inayoweza kumshawishi zaidi.

Sanchez alihusishwa sana kutaka kuhamia Juventus huku Ozil yeye Real Madrid wakitaka kumchukua tena.
Hatma ya mikataba ya Sanchez na Ozil klabuni Arsenal Hatma ya mikataba ya Sanchez na Ozil klabuni Arsenal Reviewed by Steve on Monday, September 12, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.