Propellerads

Wakala aweka wazi kwanini Pogba aliichagua Man United na kuwatosa Real Madrid



Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola ameweka wazi kwanini mteja wake
huyo aliwatosa magwiji wa Hispania Real Madrid akaenda kwa wakali wa Premier League, Manchester United.

Red Devils walimsajili nyota huyo kutoka Juventus kwa kiasi cha pauni mil 89 ambacho kilivunja rekodi.

Mourinho kupambana na Chelsea kwa Mbrazil

Inaaminika kwamba Real Madrid nao walikua wakifukuzia dili hilo, na sasa Raiola amethibitisha kwamba Pogba alitaka sehemu moja pekee.

"Hatukuongelea biashara yeyote wakati wa Euro. Alichanganyikiwa baada ya kupoteza fainali." wakala huyo aliiambia Telefoot.

"Aliniambia wazi kabisa anachokitaka. Kwa Paul, Manchester United pamekua ni nyumbani kwake daima na nilimpatia kila kilichokua kikiendelea Miami.

"Zidane pia alimtaka, nafikiri na vilabu vingine kama vitano au sita hivi."

Raiola pia amefichua kwamba Mourinho alitaka kumsajili Pogba tangu akiwa anafundisha Chelsea, lakini anadia haukuwa wakati sahihi wa kuhama.
Wakala aweka wazi kwanini Pogba aliichagua Man United na kuwatosa Real Madrid Wakala aweka wazi kwanini Pogba aliichagua Man United na kuwatosa Real Madrid Reviewed by Steve on Monday, August 29, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.