Propellerads

"Mourinho anatakiwa awajibishwe kwa anayomtendea Schweinsteiger"



Mwanachama mmoja wa ngazi za juu chama cha wachezaji Uimwenguni (FIFpro) amemtuhumu
bosi wa Man United, Jose Mourinho kwa 'kum-bully' kumnyanyasa Bastian Schwensteiger.

Mchezaji huyo mwenye miaka 32 ambaye alicheza michezo 31 ya Red Devils msimu uliopita, ameonekana kua na kia dalili za kuondoshwa kikosini tangu ujio wa Jose Mourinho majira haya.

Mwanachama wa FIFpro, Dejan Stefanovic ameanza kumshambulia Mourinho kwa kudai Mreno huyo anatakiwa apelekwe jela kwa kumlazimisha Schwensteiger kufanya mazoezi peke yake.

"Iko wazi ni unyanyasaji" aliiambia BBC "Slovenia tungemtia Mourinho hatiani na kumpa adhabu kubwa- miaka mitatu gerezani. Hii ni kumkatisha tamaa Bastian, Mourinho anaonesha mfano mbaya."

Schwensteiger hakuwemo kwenye kikosi cha Man United kilichoshinda mechi ya kirafiki dhidi ya Galatasaray iliyochezwa huko Sweden, pia hakuwepo kwenye mpambano wa juzi na Everton pale Old Trafford.
"Mourinho anatakiwa awajibishwe kwa anayomtendea Schweinsteiger" "Mourinho anatakiwa awajibishwe kwa anayomtendea Schweinsteiger" Reviewed by Steve on Friday, August 05, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.