Propellerads

Pamoja na kupoteza mchezo wa Everton, Mourinho adai hana 'pressure' yoyote!!




Kocha Jose Mourinho bado hana wasi wasi wowote huku
Chelsea ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee katika michezo mitano iliyocheza tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Mourinho alishuhudia timu yake ikipoteza  kwa 3-1 jana dhidi ya Everton, lakini bado anaamini kua kikosi chake kinacheza vizuri ukilinganisha na matokeo wanayopata.

Akiiambia Squawka, amesema " Matokeo yanakua tofauti kabisa na ubora wetu, hadhi yetu na pia tofauti na kile wachezaji wanachostahili.

"Wachezaji wanastahili zaidi ya matokeo wanayoyapata- ni rahisi sana kwa watu kunikosoa mimi na wachezaji na kila kitu lakini bado sikubaliani kabisa. Sina pressure yoyote."

Pia Mourinho aliendelea kwa kudai kua katika kuifundisha klabu ya Chelsea hamna mtu anayeweza kupamba na mikiki mikiki klabuni kama yeye.

"Mimi ni mtu wa kazi. Ni mtu ambaye nimefanya vitu vingi kwa Chelsea. Ninapat matokea ya kusononesha zaidi katika kazi yangu lakini siwalaumu wachezaji na wala sijilaumu."

Wiki ijayo Chelsea watakua na kibarua kingine watakapo wakaribisha Arsenal ambapo Chelsea kwa sasa wanatakiwa kupata ushindi ili kuwapa imani mashabiki walioanza kupoteza matumaini.
Pamoja na kupoteza mchezo wa Everton, Mourinho adai hana 'pressure' yoyote!! Pamoja na kupoteza mchezo wa Everton, Mourinho adai hana 'pressure' yoyote!! Reviewed by Steve on Sunday, September 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.