Kaseja nae avichanganya vilabu
Masaa machache baada ya TFF kumuachia huru golikipa Juma Kaseja hatimae vilabu kadhaa vimeibuka
na kutaka kumsajili masaa machache kabla ya dirisha la usajili kufungwa,vilabu vya Mwadui FC ,Mbeya City na Ndanda ya mkoani Mtwara vinapigana vikumbo sasaivi kuwania saini ya golikipa huyo.
Mtandao wa shaffihdauda.o.tz umemnukuu Juma Kaseja kama ifuatavyo.
‘ni kweli nilifanya mazungumzo na viongozi wa Mbeya City kwa ajili ya kunisajili,Mbeya City ni timu nzuri ambayo inaleta changamoto hivi sasa pia kocha wao Juma Mwambusi tunafahamuana kitambo tangu akiwa anafundisha Moro Utd,Pia leo hii asubuhi timu ya Ndanda ya mkoani Mtwara imeonyesha nia ya kunisajili hivi tunavyozungumza wakala wangu yupo nao kwenye mazungumzo’.
Timu nyingine inayomnyemelea kumsajili Kaseja ni Mwadui FC ya Shinyanga,
Kaseja nae avichanganya vilabu
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 06, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment