Propellerads

Van Gaal anatarajia nyota huyu atang'aa zaidi msimu ujao




Bosi wa mashetani wekundu, Louis van Gaal amemtaja nyota ambaye yeye anaamini
atang'aa zaidi msimu huu unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Mholanzi huyo amemtaja Luke Shaw kungaa msimu ujao ambapo amedai anaweza hata kumfunika Memphis Depay.

"Luke Shaw ni kipaji kikubwa" alinukuliwa na The Guardian

"Bado ni kijana sana, na sio rahisi kwa mtu kama yeye kutoka Southampton na kuja klabu kubwa kama Manchester United"

"Ana faida kua ni muingereza, Memphis Depay ni mholanzi, utamaduni tofauti, mchezo wao ni ladha  tofauti"

"Kwa hiyo naamini utakua ni msimu wa Luke Shaw, namuamini, na yeye anatakiwa aamini kua atafanya kweli.

"Lakini ana miaka 20. Kuna wachezaji wangapi wanaocheza Premier League wenye umri huo?"

Ili kuongeza uwezo na stamina, beki huyo wa kushoto anafanya mazoezi binafsi kipindi hiki cha mapumziko akiwa na kocha wake.

Shaw alijiunga na United msimu liopita akitokea Southampton, lakini aliweza kucheza mechi 20 pekee kutokana na kupata majeraha.

Cheki perfomance ya Luke Shaw na Januzaj hapa chini





Van Gaal anatarajia nyota huyu atang'aa zaidi msimu ujao Van Gaal anatarajia nyota huyu atang'aa zaidi msimu ujao Reviewed by Steve on Wednesday, July 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.