Propellerads

Mtazamo wa Ngoma kuhusu Kagame




Pamoja na ugumu wa mashindano, straika mpya wa Yanga, Donald Ngoma,  amesema
atahakikisha anapigana kufa na kupona ili aubakize Yanga ubingwa wa Kombe la Kagame.

Soma: Sherman atimka Yanga

Ngoma raia wa Zimbabwe aliyetokea katika timu ya Platinum FC ya nchini humo, alianza kwa mkosi michuano hiyo kwa kupata kadi nyekundu dhidi ya Gor Mahia ya Kenya  na kumlazimu kukosa mchezo mmoja, lakini aliporejea alifanya kweli na kufanikiwa kuwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya KMKM, wiki iliyopita.

Ngoma raia wa Zimbabwe amesema ana kibarua kigumu kuhakikisha anajituma ili kuonyesha kiwango na kuisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa, kwani ndiyo faraja yake.

“Nahitaji kujituma na kuonyesha kiwango katika michuano hii na katika ligi ili kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani nitafurahi sana kuona timu yangu inashinda na kutwaa ubingwa.


“Kuhusu mchezaji wa kupangwa naye uwanjani ili niweze kufiti, yeyote kati ya (Malimi) Busungu  na (Amissi) Tambwe nikipangwa naye nitafiti, kwani kinachotakiwa ni kuelewana uwanjani,” alisema Ngoma.
Mtazamo wa Ngoma kuhusu Kagame Mtazamo wa Ngoma kuhusu Kagame Reviewed by Steve on Monday, July 27, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.