Propellerads

Moshi Boban aondokewa na baba mzazi.




Mzee Moshi Shabani amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam.

Moshi ndiye
baba wa wanasoka maarufu nchini ambao ni Mrisho Moshir, Iddi Moshi ‘Mnyamwezi’, Ally Moshi na Haruna Moshi ‘Boban’.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Mnyamwezi alisema mzee wake amefariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

"Mzee katutoka, Mwenyezi Mungu amemuhitaji leo saa sita na nusu mchana. Tunatarajia mazishi yatakuwa kesho mchana, inshallah" alisema.

Marehemu ambaye alikuwa mwajiriwa wa muda mrefu wa Shirika la Reli Tanzania, amefariki baada ya kuugua muda mrefu.

Moshi Boban aondokewa na baba mzazi. Moshi Boban aondokewa na baba mzazi. Reviewed by Steve on Thursday, July 30, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.