Propellerads

Cheki Ally Kiba alivyopagawa na wakali wa Yanga




Bao la shuti kali la mita 24 alilolipiga kiungo mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya, lilimshawishi msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba kunyanyuka kwenye kiti na kushangilia.

Mwashiuya alifunga bao hilo wakati timu yake ilipovaana na Telecom ya Djibouti katika Kombe la Kagame, juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Yanga ilishinda 3-0.

Kiba alifika uwanjani hapo dakika tano baada ya mechi hiyo kuanza akiwa amevaa jezi yenye rangi ya kijani na njano namba 8 yenye jina la kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Akiwa na marafiki zake, Kiba alionekana kuwa makini kufuatilia mchezo huo huku kamera za SuperSport zikimfuatilia kwa makini.

Kiba alionekana kufurahishwa zaidi na mabao ya Malimi Busungu lakini zaidi ni lile la Mwashiuya ambapo alishangilia kwa kuruka na kupiga makofi.

Cheki Ally Kiba alivyopagawa na wakali wa Yanga Cheki Ally Kiba alivyopagawa na wakali wa Yanga Reviewed by Steve on Friday, July 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.