Messi amezungumzia jambo gumu zaidi kulifanya katika soka, unalifahamu!?
Nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi amefichua kitu ambacho
anafikiria ni kigumu zaidi kukifanya katika soka.
Kutoka kwenye kitabu kinachoitwa The Artist: Being Iniesta, Messi amempongeza mwana kikosi mwenzake Catalan, Andres Iniesta ambapo amefafanua jinsi mchezaji huyo alivyoendelea kua mzuri tangu alipokua kinda mpaka sasa.
Messi anaamini kuufanya mpira kuwa rahisi, kitu ambacho Iniesta anafanya kucheza mpira mzuri kila mchezo, ni miongoni mwa vitu vigumu kuvifanya.
"Kitu kigumu kufanya kwenye mpira ni kufanya kila kitu kionekane ni rahisi, bila juhudi sana, na huyo ndio Andres." alisema Messi.
Messi amezungumzia jambo gumu zaidi kulifanya katika soka, unalifahamu!?
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 20, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment