Huenda Luke Shaw akakaa nje tena na msimu huu kwa majeraha kutokana na tatizo hili
Beki wa Manchester United,
Luke Shaw anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina kwenye jeraha lake la muda mrefu kwenye kinena.
Beki huyo ameanza kwenye kila mchezo msimu huu lakini anahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi na madaktari wa klabu.
Shaw alitolewa nje kwenye mechi waliyopoteza kwa 3-1 mbele ya Watford Jumapili lakini alijikuta akikosolewa na meneja wake baada ya goli la pili kutokea upande wa kushoto.
Kipindi hiki kingine cha matibabu kitakua changamoto kwa Shaw kwani msimu uliopita pia alikosa mechi nyingi kutokana na kuvunjika mguu.
Huenda Luke Shaw akakaa nje tena na msimu huu kwa majeraha kutokana na tatizo hili
Reviewed by Steve
on
Monday, September 19, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment