Manchester United jana walivyopigwa Europa, Mourinho ana lipi la kujitetea!?
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho
amekataa kumtupia lawama mchezaji yoyote kufuatia kupoteza kwa 1-0 mbele ya Feyernood katika michuano ya Europa.
Red Devils walishuhudia bao la Tonny Vilhena dakika ya 11 likiwa la ushindi uwanja wa De Kuip.
Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard, bila kutajwa majina moja kwa moja walijikuta waakikosolewa na kocha huyo wa zamani wa Chelsea baada ya kupoteza kwa 2-1 dhidi ya Man City wikiendi iliyopita, lakini sasa Mourinho ameshindwa kumpa lawama mtu yeyote kwenye mchezo huu.
"Sitaki kua upande huo," aliiambia BT Sport "Sitaki kulenga mtu. Kiukweli wengine wamecheza vizuri kuliko wengine. Kwa baadhi ulikua ni mchezo wa kwanza. Tumerejea kwenye kawaida ya timu yetu bila mabadiliko mengi."
Manchester United jana walivyopigwa Europa, Mourinho ana lipi la kujitetea!?
Reviewed by Steve
on
Friday, September 16, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment