Propellerads

Kabla ya kusaini mkataba mpya, Ozil anahitaji mambo haya mawili yatimizwe kwanza




Nyota wa Arsenal, Mesut Ozil ameripotiwa kutaka
mambo mawili kwenye mkataba wake katika klabu hiyo ya London.

Gazeti la Ujerumani, Bild limedai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid bado yupo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Gunners na ana mambo mawili anayotaka kuyaona kabla hajasaini.

Kiungo huyo ambaye amekua miongoni mwa wachezaji wenye viwango vizuri tangu atue klabuni hapo mwaka 2013, ametaka jezi namba 10 na ametaka pia klabu kusaini wachezaji walio na viwango zaidi.

Inaaminika kwamba endapo akiongeza mkataba mwingine, Ozil atakua mchezaji wa kwanza Arsenal kulipwa mshahara wa pauni 200 000 kwa wiki.
Kabla ya kusaini mkataba mpya, Ozil anahitaji mambo haya mawili yatimizwe kwanza Kabla ya kusaini mkataba mpya, Ozil anahitaji mambo haya mawili yatimizwe kwanza Reviewed by Steve on Thursday, September 29, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.