Cristiano Ronaldo afunguka mipango yake ya baadaye, anataka kufanya kazi hii
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye
bado anataka kucheza kwa kiwango cha juu kwa miaka kadhaa kwa sasa amefunguka kitu gani anataka kufanya baada ya kustaafu.
Mreno huyo yupo katika mipango ya kusaini mkataba mpya Santiago Bernabeu baada ya kusisitiza anataka kustaafia katika klabu hiyo.
Sasa amefunguka kwamba atahamia upande wa umeneja pindi tu atakapotundika daruga.
"Katika miaka mitano, sita, saba ninaweza kua meneja," alisema kama alivyonukuliwa na AS.
"Kwa sasa sitaki kua meneja. Miaka michache watu watasema nina sifa nzuri lakini sitaki kua. Ni ngumu.
"Kwa sasa ninataka kukazania mpira wangu, kitu ninachopenda. Hakuna anayejua yatakayotokea baadae."
Cristiano Ronaldo afunguka mipango yake ya baadaye, anataka kufanya kazi hii
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 29, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment